FT : Yanga 0-0 (4-5)p Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Aug 2017
FT : Yanga 0-0 (4-5)p Simba
Mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya watani wa Jadi Simba na Yanga umemalizika kwa timu hizo kutoka suluhu ya 0-0 na Simba kushinda kwa mikwaju 5-4 ya penati.

Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Taifa uliishuhudia timu zote zikicheza vizuri. Licha ya kumiliki mpira kwa muda mwingi, Simba haikutengeneza nafasi nyingi za kufunga.

Kikosi cha Yanga kimeonekana kuimarika hasa sehemu ya kiungo ambapo kiungo Papi Kabamba Tshishimbi amedhihirisha ubora wake.

Tshishimbi ameonyesha ubora wake kwenye kukaba na kuanzisha mashambulizi huku akipiga pasi nyingi zinazofika sehemu husika.

Ushirikiano wake na kiungo Kamusoko utainufaisha Yanga msimu huu.



Aidha mlinzi wa pembeni Gadiel Michael naye amedhirisha hakusajiliwa na Yanga kimakosa, ameonyesha uwezo wa hali ya juu. Hakika amempa mtihani mzito Haji Mwinyi aliyekuwa amejimilikisha nafasi hiyo.

Walinzi wa kati Yondani na Dante licha ya makosa madogo madogo yaliyojitokeza, wanaweza kutengeneza pacha nzuri na kuondoa kabisa hofu kwenye safu ya ulinzi.

Kwa ujumla Yanga imecheza vizuri, kuanzia mlinda lango Youthe Rostand, Emanuel Martin, Ibrahim Ajib, Donald Ngoma na Raphael Daudi wametimiza wajibu wao ipasavyo kama walivyoelekezwa na mwalimu wao.



Leo tumeshuhudia wachezaji wote wakiwa wepesi kwenye kuziba nafasi.

Kikosi kimeonekana kiko imara, kukosekana kwa mshamuliaji Amissi Tambwe ambaye ni majeruhi kumeiathiri safu ya ushambuliaji.



Mchezo huo ulikuwa ni lazima mshindi apatikane, mara nyingi penati ni bahati. Tumepoteza kwa mikwaju ya penati lakini vijana wanastahili pongezi kwa kazi kubwa waliyoifanya leo.

Waliofunga mikwaju ya penati.

YANGA
1.Yondani (KOSA)
2.Tshishimbi (PATA)
3. Kamusoko (PATA)
4. Ajibu (PATA)
5. Ngoma (PATA)
1. Mahadhi (KOSA)

SIMBA
1. Mwanjale (PATA)
2. Okwi (PATA)
3. Niyonzima (PATA)
4. Kichuya (PATA)
5. Zimbwe (KOSA)
1. Mo Ibrahim (PATA)
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’