Wachezaji Yanga wampagawisha Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Dec 2018
Wachezaji Yanga wampagawisha Zahera
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewapongeza wachezaji wa timu hiyo kwa kuendelea kufanya vizuri katika ligi kuu ya Tanzania Bara.

Yanga iko kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya kujikusanyia alama 35 kutoka michezo 13.

Zahera raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema wachezaji wa Yanga wanastahili pongezi kwa mafanikio wanayopata hasa katika kipindi hiki ambacho Yanga inapita

"Wachezaji wamekuwa wakijituma sana, wanastahili pongezi kwa mafanikio haya. Sasa tunaongoza ligi, ni wachache sana waliofikiria kama Yanga itaweza kuwa nafasi hii," amesema Zahera

β€œTutapambana kuhakikisha tunaendelea kubaki kileleni. Nataka wachezaji wangu wajitume zaidi kwenye kila mchezo kuhakikisha tunaendeleza rekodi yetu ya kutopoteza mchezo wowote, kila mchezo mmoja tunapomaliza tunajipanga kwa mchezo mwingine,” alisema Zahera.

Yanga licha ya kupitia katika kipindi kigumu nje na ndani ya uwanja, bado imeenedelea kufanya vizuri ambapo mpaka sasa haijapoteza mchezo wowote kwenye ligi hiyo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’