Mahakama Kuu ya Dar es Salaam imetengua maamuzi ya Kamati za Maadili za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumfungia maisha aliyekuwa Makamu wa Rais, Michael Richard Wambura.
Uamuzi huo umetolewa leo katika mahakama hiyo na Jaji, Dk. Benhajji Masoud kufuatia kesi iliyofunguliwa na Wambura kupinga kufungiwa maisha na Kamati za Maadili za TFF.
Kwa uamuzi huo, Wambura anarejea katika madaraka yake ya Umakamu wa Rais wa TFF na Uenyekiti wa Chama cha Soka Mara (FAM).
Aidha, Athumani Nyamlani aliyekuwa anakaimu nafasi hiyo sasa anapoteza wadhifa huo aliopewa baada ya kuwa Mjumbe Mteule wa Kamati ya Utendaji.
cc Bin Zubeiry

ADVERTISE HERE