Sikugoma, nasumbuliwa na enka - Yondani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
30 Nov 2018
Sikugoma, nasumbuliwa na enka - Yondani
Nahodha wa Yanga Kelvin Yondani amevunja ukimya baada ya kuwa nje tangu arejee nchini na kikosi cha timu ya Taifa kutoka Lesotho

Yondani amekanusha taarifa zilizotolewa kuwa aligoma kuitumikia Yanga akishinikiza alipwe malimbikizo ya mishahara.

Amebainisha kuwa alipata majeraha wakati akiitumikia timu ya Taifa hivyo kushindwa kusafiri na timu kanda ya ziwa

“Ilikuwa ngumu kwangu mimi kusafiri na timu nikiwa nina majeraha na isitoshe mazingira mabaya ya viwanja hivyo tulivyokuwa tunakwenda kuvichezea mechi ni lazima ningejitonesha na kusababisha majeraha kuwa makubwa zaidi, Yondani amenukuliwa na gazeti la Sport Xtra

“Siwazuii watu kuongea, waache waongee tu lakini ukweli ni huu sababu iliyonifanya nishindwe kusafiri na timu kanda ya ziwa, mimi nilijitonyesha enka nikiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa lakini nashukuru hivi sasa naendelea vizuri baada ya kuanza matibabu.

“Nikiri ni kweli kabisa mimi ninawadai Yanga, lakini sijagoma na unanijua vizuri jinsi ninavyokuwa nikiwa ninadai haki yangu na ningekuwa nimegoma, basi nisingetokea mazoezini leo (juzi), hivyo niwaondoe hofu mashabiki wa Yanga.

“Kama Mungu akipenda nitakuwepo kwenye mchezo ujao wa ligi kama maendeleo yangu yakiwa mazuri, lakini ninaamini huu ndiyo muda muafaka kwa wadogo zangu akina Ninja nao kuonekana kwani wana uwezo mzuri"

Yondani amekosa michezo yote mitatu iliyopita ambayo Yanga imeibuka na ushindi.

Hakusafiri kwenda mkoani Shinyanga kuikabili Mwadui Fc, mkoani Kagera dhidi ya Kagera Sugar na jana uwanja wa Taifa dhidi ya JKT Tanzania.

Hata hivyo kikosi cha Yanga kimeonyesha kuwa imara hata bila ya uwepo wake pamoja na mlinda lango Beno Kakolanya ambaye pia amesharejea kikosini
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →