Buswita afungiwa mwaka mmoja

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Aug 2017
Buswita afungiwa mwaka mmoja
Saa chache kuelekea mpambano wa watani wa jadi, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemfungia kiungo wa Yanga Pius Buswita mwaka mmoja kwa kosa la kusaini mikataba na timu mbili tofauti yaani Simba na Yanga.

Hayo yameweka wazi baada ya kikao cha Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inayoongozwa na Wakili Richard Sinamtwa, ambayo ilikutana Agosti 20 mwaka huu Jijini Dar es Salaam kupitia usajili wa majina ya klabu 40 uliyofanywa katika kipindi cha usajili.

Kamati hiyo ilibaini kwamba mchezaji huyo aliyechezea Mbao FC ya Mwanza msimu uliopita Pius, amevunja Kanuni ya 66 ya usajili Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo inaelekeza adhabu ya kufungiwa mwaka mmoja.

Cha kushangaza Busitwa hakuwemo kwenye orodha ya wachezaji iliyowasilishwa na klabu ya Simba TFF. Anasemekana kasajiliwa na timu mbili lakini hakuna timu iliyowasilisha jina TFF zaidi ya Yanga.

Tutarajie uongozi wa Yanga kukatia rufaa maamuzi haya.

Aidha huu haukuwa wakati muafaka kwa TFF kuchukua maamuzi kama hayo.

TFF ingeweza kufanya maamuzi hayo mapema kuliko ilivyofanya sasa ikifahamu tayari maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Jamii yameshakamilika, Buswita akiwa sehemu ya kikosi cha Yanga.

Upo uwezekano mkubwa wa kitendo hichi kufikiriwa kama 'hujuma' kwa klabu ya Yanga.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
26m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’