Ngasa anaendelea kutoa majibu 'mbashara'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Nov 2018
Ngasa anaendelea kutoa majibu 'mbashara'
Mrisho Ngasa ni kama amezaliwa upyaaaa kwani mambo anayofanya dimbani sio ya kawaida. Leo amefunga bao lake la nne msimu huu akitupia katika michezo miwili mfululizo.

Anachokifanya Ngasa sasa ni kuwapa majibu 'mbashara' wale wote waliokuwa wanam-beza na kusema umri umemtupa mkono.

Amekuwa na ushirikiano mzuri sana na Heritier Makambo ambaye kasi yake ya kupachika mabao tayari imeanza kuwatia hofu upande wa pili

Amefikisha mabao saba na inaonekana atafunga sana msimu huu.

Makambo ni mshambuliaji aliyekamilika, amedhihirisha hilo na anao uwezo wa kufunga aina zote za mabao.

Kwa hakika kikosi cha Yanga sasa kimeiva.

Licha ya changamoto za nje ya uwanja, wachezaji wa Yanga wamekuwa wakicheza kwa kujituma, Na sasa kuna kitu kingine kimeongezeka, WANAJIAMINI

Ile burudani ya 'kampa-kampatena' imeanza kurejea. Sasa Yanga inapata ushindi huku pia ikicheza mpira 'mwingi' tofauti na ilivyokuwa mwanzoni mwa msimu

Yanga hii itawashangaza wengi msimu huu..
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’