Saa chache zijazo kikosi cha mabingwa kihistoria Tanzania, Yanga kitashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili JKT Tanzania kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kuanzia saa kumi kamili jioni na sio saa 12 kama ilivyotaarifiwa awali.
Yanga imekuwa na msimu mzuri mpaka sasa ikiwa imeshuka dimbani mara 12 na kujikusanyia alama 32 baada ya kushinda michezo 10 na kutoka sare michezo miwili.
Ikiwa haijafungwa kwa zaidi ya miezi mitatu, Yanga itashuka dimba la Taifa leo na malengo ya kuilinda rekodi hiyo ambayo haikutarajiwa na wengi.
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amewataka mashabiki wa timu hiyo wajitokeze kwa wingi uwanja wa Taifa kuipa sapoti timu yao ili iweze kuibuka na ushindi.
Ushindi utaipeleka Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi.
Viingilio vya mchezo huo;
VIP A - 15,000/-
VIP B na C - 10,000/-
Mzunguuko - 5,000/-

ADVERTISE HERE