Kabwili kuibeba Yanga dhidi ya JKT Tanzania leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Nov 2018
Kabwili kuibeba Yanga dhidi ya JKT Tanzania leo
Licha ya kurejea kikosini, mlinda lango namba moja wa Yanga Beno Kakolanya hatacheza mchezo wa leo dhidi ya JKT Tanzania baada ya kukosa mazoezi ya timu hiyo kwa siku kadhaa.

Jana kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera alithibitisha kuwa Kakolanya ni miongoni mwa wachezaji ambao wataukosa mchezo wa leo unaotarajiwa kuanza saa 12 jioni.

Wengine wanaotarajiwa kukosa mchezo huo kutokana na majeruhi ni Gadiel Michael, Juma Mahadhi, Baruani Akilimali na Kelvin Yondani

Kiungo Papi Tshishimbi naye ataukosa mchezo huo licha ya kuwa amerejea kikosi lakini bado hayuko 'fit'

Kukosekana kwa Kakolanya kunatoa nafasi nyingine kwa mlinda lango kinda Ramadhani Kabwili kukaa golini mbele ya Mcongomani Klaus Kindoki.

Kindoki amepoteza imani ya benchi la ufundi kwake baada ya kufanya makosa yaliyopelekea kuizawadia bao Mwadui fc kwenye mchezo wa ligi wiki iliyopita.

Makosa kama hayo aliyafanya kwenye mchezo wake wa kwanza msimu huu dhidi ya Stand United uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 4-3'

Moja ya mabao ya Stand ambayo yote yalifungwa na Alex Kitenge, lilitokana na kosa la kutema mpira.

Kindoki ameonekana kuwa na 'mchecheto' mwingi anapokuwa langoni.

Kabwili alicheza dakika 45 za kipindi cha pili dhidi ya Mwadui Fc na kudaka dakika zote 90 kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar

Kabwili amedhihirisha anaweza kumpa changamoto Beno na leo ni nafasi nyingine kwake.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’