Sita kuikosa JKT Tanzania kesho

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Nov 2018
Sita kuikosa JKT Tanzania kesho
Kikosi cha Yanga kesho Alhamisi kitashuka kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuikabili JKT Tanzania katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 12 jioni.

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema wamejiandaa kikamilifu kuikabili JKT Tanzania ambayo inatambulika kwa kucheza mpira wa nguvu.

"Tumejiandaa vyema na najua kama tunaenda kutana na timu ambayo ina physic sana ila kwa jinsi nilivyoiandaa timu yangu naamini wakifuata yale yote niliowafundisha basi mwisho wa dakika 90 ntapata pointi tatu kwenye mchezo huo," amesema Zahera

Aidha Zahera amebainisha wachezaji sita wataukosa mchezo huko kutokana na sababu mbalimbali.

"Wachezaji Gadiel Michael, Kelvin Yondani,Juma Mahadhi pamoja Baruan Akilimali bado wanasumbuliwa na majeraha na hawatokuwa sehemu ya mchezo wa kesho"

"Papy Tshishimbi yeye tayari ameanza mazoezi lakini bado hajawa sawa hivyo nae pia siwezi kumtumia kwenye mchezo wa kesho pamoja na golikipa Beno Kakolanya"
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
37m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’