Msimu ujao timu 20 kushiriki VPL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Aug 2017
Msimu ujao timu 20 kushiriki VPL
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litapandisha idadi ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu msimu ujao wa 2018/19 kutoka 16 za sasa hadi 20, imefahamika.

Uamuzi huo umefanyika Jumanne Agosti 22, 2017 wakati Kamati ya Utendaji inafanya marekebisho ya Kanuni za Ligi Daraja la Kwanza inayotarajiwa kuanza Septemba 16, mwaka huu.

Kwa marekebisho hayo, timu zitakazoshuka daraja msimu ujao kutoka Ligi Kuu ya Vodacom ya sasa ni mbili hivyo kubaki 14.

Na ili kufikia timu 20, timu sita (6) za Ligi Daraja la Kwanza zitapanda daraja.

Kwa mujibu wa utaratibu wa Ligi Daraja la Kwanza, ina maana kwamba msimu huu timu mbili zitapanda kutoka katika kila kundi katika ligi hiyo ambayo inatarajiwa kuanza Septemba 16, mwaka huu.

Makundi ya Daraja, kundi Γ’β‚¬ΛœAÒ€ℒ lina timu za African Lyon, Ashanti United, Friends Rangers za Dar es Salaam, JKT Ruvu na Kiluvya United za Pwani, Mgambo JKT ya Tanga, Mvuvumwa ya Kigoma na Polisi Moro ya Morogoro.

Kundi Γ’β‚¬ΛœBÒ€ℒ ziko za Coastal Union ya Tanga; JKT Mlale ya Ruvuma; KMC ya Dar es Salam, Mawezi Market ya Morogoro, Mbeya Kwanza ya Mbeya, Mufundi United ya Iringa, Mshikamano na Polisi Dar za Dar es Salaam.

Kundi Γ’β‚¬ΛœCÒ€ℒ lina timu za Alliance School, Pamba na Toto
African za Mwanza, Rihno Rangers ya Tabora, Polisi Mara ya Mara, Polisi Dodoma ya Dodoma, Transit Camp ya Shinyanga na JKT Oljoro ya Arusha.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
33m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’