Mkwasa aipa neno TFF kuhusu uchaguzi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
27 Nov 2018
Mkwasa aipa neno TFF kuhusu uchaguzi Yanga
Katibu Mkuu wa zamani wa Yanga Charles Mkwasa amelitaka Shirikisho la soka Tanzania (TFF) litumie busara kumaliza sintofahamu iliyojitokeza juu ya uchaguzi wa klabu ya Yanga hasa nafasi ya Mwenyekiti

Mkwasa amesema licha ya kuwepo kwa upungufu mbalimbali wa kikatiba juu ya suala hilo, TFF inapaswa kutumia busara ili kuhakĀ­ikisha Yanga inakuwa sawa na siyo kusababisha mvurugano.

ā€œKama Manji amekubali kurudi katika nafasi yake ya uongozi kutokana na uamuĀ­zi wa wanachama wa Yanga walioutoa kwenye mkutano mkuu wa klabu uliofanyika mwezi Juni, mwaka huu, TFF inapaswa kukubaliana na maamuzi hayo kwani hata katiba ya klabu inaseĀ­ma kuwa wenye maamuzi ya mwisho juu ya jambo lolote lile ni wanachama kupiĀ­tia mkutano mkuu," Mkwasa amenukuliwa na gazeti la Championi

ā€œNakumbuka katika mkuĀ­tano huo, mimi ndiye niĀ­likuwa katibu ambapo wanachama kwa pamoja waliikataa barua ya kujiuĀ­zulu ya Manji na wakanitaka niwaandike barua ya kutaarĀ­ifu kuhusiana na uamuzi wao huo, nilifanya hivyo na barua nyingine nikaipeleka TFF na katika mamlaka nyĀ­ingine.

ā€œBaada ya TFF kuiĀ­pokea barua hiyo ilibidi wamwondoe aliyekuwa KaiĀ­mu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, kutokana na maamuzi ya mkutano mkuu wa klabu yaliyofanywa na wanachĀ­ama ya kugomea barua ya kujiuzulu kwa Manji, kwa hiyo hana sifa za kuwa katika nafasi hiyo kwa sababu Manji bado ni mwenyekiti Yanga.

ā€œKwa hiyo kutokana na hali hiyo, TFF inapaswa kutumia busara kulimaliza tatizo hilo kwa faida ya soka la Tanzania hata kama kuna upungufu wa kikatiba amĀ­bao haukufuatwa ambao wao ndio wanasimamia laĀ­kini mwisho wa siku wenye maamuzi ya Yanga ni Yanga wenyewe, tena kupitia mkuĀ­tano wao mkuu,ā€ amesema

Wakati Yanga ikipinga uchaguzi wa nafasi hiyo baada ya Mwenyekiti wake Yusufu Manji kuandika barua ya kukubali kurejea kuiongoza timu hiyo, TFF kupitia Kamati yake ya uchaguzi imeendelea na mchakato wa uchaguzi licha ya kususiwa na Yanga.

Kamati ya uchaguzi ya TFF inayoongowa na Wakili Malangwe Mchungahela tayari imetangaza majina ya wagombea 23 wenye sifa za kuwania nafasi hizo baada ya kufungwa kwa mchakato wa kutoa na kurudisha fomu Novemba 19

Hata hivyo mchakato huo umekosa 'baraka' za viongozi wa Yanga baada ya kuususia wakishikilia msimamo wa kumtambua Manji kama Mwenyekiti halali na kutaka uchaguzi huo usimamiwe na Yanga yenyewe.

Hata fomu za wagombea hao zilitolewa na TFF huku Yanga ikigoma kuwapigia mihuri ya klabu wagombea waliofika Makao Makuu ya klabu hiyo.

Aidha fomu hizo pia hazikusainiwa na viongozi wa Yanga
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE →