Yanga yapania kuendeleza wimbi la ushindi Kagera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Nov 2018
Yanga yapania kuendeleza wimbi la ushindi Kagera
Safari ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu inatarajia kuendelea kwa Kagera Sugar kuwakaribisha Yanga kutoka jijini Dar es Salaam katika mchezo utakaochezwa leo kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Katika mechi hiyo ya kiporo, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, huenda akamuanzisha golikika kijana, Ramadhani Kabwili baada ya kukosekana kwa Benno Kakolanya huku Kindoki akionekana kukosa kujiamini

Kabwili aliingia kipindi cha pili katika mchezo uliopita dhidi ya Mwadui FC ambao Yanga waliibuka na ushindi wa magoli 2-1.

Zahera, amesema kuwa amejipanga vyema kuhakikisha anatimiza malengo yake ya kuvuna pointi sita kwenye michezo mwili ya Kanda ya Ziwa.

"Nashukuru tumefanikiwa kupata ushindi katika mchezo wa kwanza kule Shinyanga, japo haukuwa mchezo mwepesi, tumejipanga kwa ajili ya kushinda pia dhidi ya Kagera ingawa kuna mchezaji kama Gadiel (Michael) ambaye ameumia, tutamkosa," Zahera amenukuliwa na gazeti la Nipashe Jumapili

Kocha huyo aliongeza kuwa ana uhakikia wachezaji wake watafanya kile walichokifanya katika mchezo uliopita na kuendelea kujiweka katika mazingira mazuri ya kuwania ubingwa wa ligi ambao unashikiliwa na watani zao, Simba.

"Kutakuwa na mabadililo kidogo ambayo siwezi kusema, nataka tufikie malengo yetu ya kuvuna pointi sita huku ugenini, najua si kazi rahisi, tumejiandaa kwa changamoto zote," Zahera aliongeza.

Naye Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime, alisema Yanga wasitarajie mteremko katika mchezo wa leo kwa sababu nao wamejipanga kuondoka na ushindi kwenye uwanja wa nyumbani.

"Tumejiandaa, kama mwalimu nasema kila kitu kipo sawa, tunasubiri tu mchezo, Yanga ni timu nzuri na inafanya vyema lakini hatuwaogopi, tumejipanga kufanya vizuri katika uwanja wetu wa nyumbani ili kuwafurahisha mashabiki wetu," alisema Maxime.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’