Wakati uongozi wa klabu ya Yanga ukiendelea na maandalizi ya Mkutano Mkuu wa dharura utakaofanyia Disemba 01 katika ukumbi ambao utatangazwa baadae, jana Shirikisho la soka nchini (TFF) lilianza kuwafanyia usaili wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika klabu ya Yanga.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliyopanga kusimamia uchaguzi wa Yanga, jana Ijumaa iliwafanyia usaili wagombea mbalimbali wakiwemo wanne wanaogombea nafasi ya mwenyekiti, wanne nafasi ya makamu mwenyekiti na wajumbe 16.
Katika nafasi ya Mwenyekiti wanaogombea ni Jonas Tiboroha, Mbaraka Igangula na Erick Ninga wakati wagombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Titus Ossoro, Salum Chota, Yono Kevela na Pindu Luhoyo
Yanga imepanga kufanya Uchaguzi Mkuu Januari 13 lakini wakitaka kujaza nafasi nyingine zote kasoro ya Mwenyekiti.
Klabu hiyo bado imendelea kushikilia msimamo wake wa kumtambua, Yusuf Manji kuwa mwenyekiti wake huku Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likidai halimtambui.
Moja ya ajenda za Mkutano Mkuu wa dharura ni suala la uchaguzi huo

ADVERTISE HERE