Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ametaja sababu ya kutompanga kinara wa kutengeneza mabao Ibrahim Ajib kwenye mchezo wa leo dhidi ya Mwadui Fc licha ya mchezaji huyo kusafiri mkoani Shinyanga.
Zahera amesema Ajib hakuwa akihudhuria mazoezi siku zote katika kipindi cha wiki mbili ambazo yeye alikuwa Congo kutimiza majukumu ya timu ya Taifa.
Aidha Zahera amesema katika michezo mitatu ya kirafiki ambayo Yanga imecheza Ajib alihudhuria mchezo mmoja tu.
"Nilipoondoka kwenda Congo nilimuachia kocha msaidizi program za mazoezi na alikuwa akinipa taarifa ya maendeleo kila siku usiku"
"Katika siku 13 ambazo sikuwepo, Ajib hakufika mazoezini karibu mara nne au tano. Pia katika michezo mitatu ya kirafiki tuliyocheza Ajib hakutokea kwenye michezo miwili"
"Mimi nikasema hata akija mazoezini baada ya mimi kurudi siwezi kumchezesha mtu asiyefanya mazoezi. Ni bora nifungwe nikiwa na wachezaji wenye nidhamu na wanaotimiza majukumu yao vyema," amesema Zahera

ADVERTISE HERE