Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera anaamini timu yake itafanya vizuri kwenye mchezo wa leo dhidi ya Mwadui Fc licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji.
Zahera amesema amekuwa akiiandaa timu yake katika mazingira yoyote kuepuka utegemezi wa mchezaji mmoja mmoja ambapo mchezaji huyo akikosekana timu inayumba.
"Tumecheza mechi karibu tatu bila ya Ajib, tumecheza mechi mbili bila ya Kelvin Yondani," Zahera ameiambia Yanga TV
"Nimewaambia wachezaji wangu, mmoja anapokosekana, ni nafasi kwa mchezaji mwingine kufanya vizuri ili aweze kuwemo kikosini michezo ijayo"
"Sitaki kuwapa kichwa wachezaji wangu kuwa timu haiwezi kufanya vizuri kama wasipokuwepo. Wakiwepo ni vizuri lakini hata wasipokuwepo wapo wengine wa kucheza nafasi zao"
"Napenda nishindwe nikiwa na wachezaji ambao wanafanya mazoezi kila siku. Nishindwe nikiwa na wachezaji ambao wenyewe wanajituma," amesema.

ADVERTISE HERE