Wachezaji wote wana madai Yanga, kugoma sio suluhu - Kaya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Nov 2018
Wachezaji wote wana madai Yanga, kugoma sio suluhu - Kaya
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omary Kaya amesema hana taarifa ya kilichopelekea nahodha Kelvin Yondani na mlinda lango Beno Kakolanya kushindwa kufariri kwenda mkoani Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Mwadui Fc leo.

Kaya amesema Yanga itatoa taarifa baada ya kuonana na wachezaji hao lakini kwa sasa mengi yanayozungumzwa yanabaki kuwa tetesi tu

"Mimi sijapata kauli ya Beno wala Kelvin, kwa hiyo kama ni majeruhi nitapata ripoti kutoka timu ya taifa ambayo itakwenda kwa daktari wetu," amesema Kaya

"Kama itakuwa ni sababu nyingine pale nitakapokutana nao au kupata taarifa kutoka sehemu husika nitazungumza hilo lakini sidhani kama ni jambo la busara kumsemea mtu

"Yanga timu nzima inadai, kama ni suala la kudai inawezekana tatizo likawepo hata mimi naweza kusema nadai lakini kitu cha kwanza sio kugoma, ni kufanya kazi yangu na kufata taratibu muhimu za kupata stahiki yangu.

"Kwa hiyo watu wasipende kuzungumza kitu wasichokuwa na uhakika nacho lakini siwezi kumzuia mtu kusema kwa sababu kila mtu anazungumza chochote anauhuru huo ila kiofisi hakuna barua iliyokuja wala kauli ya Beno au Kelvin akisema siendi huko, nitakuwa naongopa", amesema

"Kimsingi ni kweli hawajaenda na timu lakini siwezi kusema ni kwa sababu gani kwani bado sijapata mawasiliano yao lakini ilikuwa waje waunganishe

"Inawezekana labda mtu ana udhuru wa kifamilia lakini ni hadi watakapopatikana na kusema ndio tutajua nini kitafuata baada ya hapo," amesema kaya

Jana kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera alisema wachezaji hao hawakupatikana hewani baada ya kuzima simu zao muda mfupi baada ya kuwasili kutoka Lesotho walikokuwa na timu ya Taifa

"Viongozi waliwapigia simu hawakupatikana basi mimi nikawaambia waacheni msiwapigie tena simu," alisema Zahera.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’