Kikosi cha Yanga kiko mkoani Shinyanga tangu jana Jumanne ambapo leo jioni kimefanya mazoezi yake ya mwisho kwenye uwanja wa CCM Kambarage utakaopigwa mchezo dhidi ya Mwadui Fc hapo kesho.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera alikuwepo dimbani leo kusimamia mazoezi hayo sambamba na kocha msaidizi Noel Mwandila na Meneja Nadir Haroub 'Cannavaro'
Zahera alitua jana usiku kutoka DR Congo kabla ya kuunganisha moja kwa moja mkoani Mwanza na baadae Shinyanga kuungana na kikosi cha Yanga.
Yanga itashuka dimbani kesho kucheza mchezo wake wa kwanza nje ya jiji la Dar es salaam ikiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo.
Matokeo ya ushindi hapo kesho yataipandisha Yanga hadi nafasi ya pili mbele ya Simba ambayo itashuka dimbani keshokutwa Ijumaa dhidi ya Lipuli Fc.
Meneja wa Yanga Nadir Haroub amesema timu iko imara na wana matumaini makubwa ya kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wa kesho.

ADVERTISE HERE