Zahera hauhofii uwanja wa Kambarage

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Nov 2018
Zahera hauhofii uwanja wa Kambarage
Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga ambao utatumika kwenye mchezo wa kesho kati ya Mwadui Fc dhidi ya Yanga unafahamika hali yake sio ya kuridhisha.

Lakini hilo halimuumizi kichwa kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ambaye amesema amekiandaa kikosi chake kucheza katika mazingira ya viwanja 'vikorofi'.

"Tumekuwa tukifanya mazoezi kwenye uwanja ambao sio mzuri. Tumefanya hivyo kwa sababu tunatambua viwanja vingi hapa nchini sio vizuri," amesema Zahera.

Zahera amesema anaamini vijana wake watapambana kuhakikisha wanapata matokeo kwenye mchezo wa kesho.

Kuhusu kukosekana kwa nahodha Kelvin Yondani na Beno Kakolanya, Zahera amesema wapo wachezaji ambao watacheza katika nafasi zao.

Zahera amesema wachezaji hao wameshindwa kusafiri na wachezaji wengine kutokana na kuwa na mgogoro na uongozi wa Yanga.

"Wachezaji hao walisema hawawezi kusafiri sababu ya uchovu jambo ambalo sio sahihi. Fei Toto na Gadiel mbona wamesafiri na walikuwa na timu ya Taifa?" amehoji Zahera

"Walipofika walizima simu zao viongozi wamejaribu kuwatafuta bila ya mafanikio, mimi nikawaambia waacheni, msiwapigie simu"
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’