Kiungo wa Yanga, Feisal Salum 'Fei Toto', amesema pamoja na matokeo mabaya waliyoyapata akiwa na kikosi cha timu ya Taifa 'Taifa Stars' kwenye mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2019 dhidi ya Lesotho, sasa anaelekeza nguvu na akili kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mwadui FC.
Kesho, Yanga inashuka kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga kucheza mchezo wao wa kiporo.
Wachezaji wa Yanga waliokuwapo kwenye kikosi cha Stars, Fei toto na Gadiel Michael, wapo Shinyanga na wenzao tayari kwa kuwakabili wapinzani wao hao.
Kuelekea mchezo huo Fei Toto amesema kwa sasa anaelekeza nguvu kwenye mchezo huo ili aisaidie Yanga ipate pointi tatu muhimu.
βKwa sasa tunaelekeza akili kwenye mchezo wa Ligi Kuu..., tunacheza ugenini, lakini lengo letu ni ushindi na tutapambana kuhakikisha hatupotezi,β Fei Toto amenukuliwa na gazeti la Nipashe
Amesema anafahamu michezo ya ugenini ina changamoto nyingi, lakini watafuata mbinu na maelekezo ya benchi lao la ufundi kuweza kuendeleza rekodi yao ya kutofungwa mpaka sasa
Baada ya mchezo huo, Yanga watasafiri kutoka Shinyanga kwenda Bukoba mkoani Kagera kuvaana na Kagera Sugar Jumapili ijayo.

ADVERTISE HERE