Baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Ally Mchungahela kusema zoezi la kuchukua na kurejesha fomu limefungwa rasmi na keshokutwa Ijumaa utafanyika mchujo kwa wagombea wote, klabu ya Yanga imeshauriwa kuwa inapaswa kuiga mfumo wa timu kubwa kama Barcelona na Real Madrid au ikibidi iige majirani zao Simba.
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa, Kanali mstaafu, Iddi Kipingu amesema kiongozi atakayechaguliwa anapaswa kuwa na uwezo wa kuhakikisha klabu inakuwa na vyanzo vingi vya mapato, lakini siyo kutegemea fedha kutoka mfukoni kwa mtu.
"Dunia ya sasa kila kitu kinaeleweka, hakuna asiyefahamu timu kama Barcelona, Real Madrid na nyinginezo za wananchi zinaongozwaje, bahati nzuri hapa nchini, Simba imeanza hivyo hata bila Manji kama Yanga wakiamua watafika kwenye mafanikio wanayohitaji," alisema.
Yanga inatarajiwa kufanya uchaguzi wa kuziba nafasi zilizo wazi ikiwamo ya Mwenyekiti iliyokuwa ikishikiliwa na Manji ambaye aliomba kujiuzulu mwaka jana lakini hivi karibuni Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini, George Mkuchika alisema Manji yupo na ataripoti rasmi ofisini Januari 15 ikiwa ni siku mbili baada ya uchaguzi huo wa Januari 13.
Hata hivyo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilipinga kauli hiyo ya Mkuchika na kusisitiza kwamba kama Yanga wanahitaji Manji arejee basi wamchukulie fomu agombee tena, lakini hadi Juzi Jumatatu wakati pazia la kuchukua na kurejesha fomu likifungwa jina la Manji alikuwepo kwenye orodha ya waliochukua fomu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Ally Mchungahela alisema zoezi la kuchukua na kurejesha fomu limefungwa rasmi na keshokutwa Ijumaa utafanyika mchujo kwa wagombea wote.
"Uchaguzi huko pale pale kwa wagombea waliochukua fomu, baada ya mchujo Ijumaa, kutakuwa na usaili kisha wagombea wataingia kwenye kampeni kuelekea kwenye uchaguzi huo," alisema Mchungahela.
Aidha 'bosi' huyo wa kamati ya uchaguzi alitoa onyo kwa yoyote atakayejaribu kujipenyeza kuvuruga mchakato wa uchaguzi kwa kuanzisha vurugu akisisitiza kuwa vyombo vya dola vitafanya kazi yake.
Wakati Yanga ikitarajiwa kupata viongozi wapya, baadhi ya wadau wa soka wamewashauri Wanachama wa klabu hiyo kubadili fikra ya kumtegemea mtu na badala yake waamini mfumo bora ndiyo utawafikisha kwenye mafanikio wanayoyahitaji.
Mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Ally Mayay alisema kikubwa ni wana Yanga kukubali mabadiliko, kwani hayakwepeki, japo wasiwasi upo kutokana na maisha ya Yanga wakati wa Manji.
"Yanga hawana namna, inabidi wakubaliane na hali halisi, huu ni wakati wa kutegemea mfumo na si kumtegemea mtu, 'solution' kwao ni kuwa na mfumo ambao hata Manji asipokuwepo mfumo utaiweka klabu katika mazingira salama," alisema Mayay.
Wakati mmoja kati ya Dk Jonas Tiboroha, Yono Kavela, Titus Osoro au Baraka Igangula akisubiriwa kukabidhiwa kijiti cha Yusuf Manji.
Kwenye uchaguzi huo, nafasi nyingine zitakazozibwa ni ile ya makamu mwenyekiti inayogombewa na Kavela na Osoro ambao walichukua fomu pia kwenye nafasi ya mwenyekiti, wakati wajumbe ni Mussa Katabalo, Salim Seif na Benjamin Jackson.
Wengine ni Pindu Luloya, Sylvester Haule, Hamad Islam, Shaffii Amri, Said Baraka, Dominic Francis, Ally Msigwa, Leonard Malongo, Salum Chota, Ramadhan Said, Geofrey Mwita, Faustine Mabula, Frank Kalokola na Arafati Haji.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE