Wakati Yanga ikiwa mkoani Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara kesho dhidi ya Mwadui Fc, nahodha Kelvin Yondani na mlinda lango Beno Kakolanya hawakusafiri na timu hiyo jana ambapo inadaiwa wawili hao wamegoma wakishinikiza walipwe malimbizo ya mishahara na fedha za usajili.
Matukio haya ya migomo ndiyo yaliyopelekea Yanga kufanya vibaya michezo yote ya mikoani mwishoni mwa msimu uliopita.
Wakati huu ambao Yanga inakabiliwa na changamoto hizi ndio ilitarajiwa wale wote wanaojisemea kwenye vyombo vya habari kuwa na mapenzi na Yanga kujitokeza hadharani kusaidia.
Ni bahati mbaya hakuna hata mmoja ambaye atajitokeza lakini watakaposikia kuna mchakato wowote wa kumrejesha Manji Yanga ndio watasikika tena.
Migomo hii ya mapema ni dalili mbaya kwa Yanga ambayo moja ya mikakati yake ni kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu.
Pia si dalili nzuri kwa mpango wa uboreshaji wa kikosi wakati huu wa dirisha dogo la usajili.

ADVERTISE HERE