Wagombea 27 wajitokeza kuwania uongozi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Nov 2018
Wagombea 27 wajitokeza kuwania uongozi Yanga
Zoezi la kuchukua na kurudisha fomu za kuwania nafasi za uongozi katika klabu ya Yanga limefungwa rasmi juzi ambapo wagombea 27 wamejitokeza kuwania nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na nafasi nne za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

Mwanasheria wa TFF Herman Kidifu amesema wagombea wanne wamejitokeza kuwania nafasi ya Mwenyekiti ambao ni Dk Jonas Tiboroha, Yono Kevela, Mbaraka Igangula na Erick Ninga.

Waliochukua fomu za kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Titus Osoro, Salum Magege Chota na Kevela.

Wajumbe ni Hamad Ally Islamu, Benjamin Jackson Mwakasonda, Sylvester Haule, Salim Seif, Musa Katabaro, Shftu Amri na Said Baraka.

Wengine ni Pindu Luhoyo, Dominick Francis, Seko Jihadhari, Ally Omary Msigwa, Arafat Ally Haji, Geofrey Boniphace Mwita, Frank Kalokola, Ramadhan Said, Leonard Marango, Bernard Faustin Mabula, Christopha Kashiririka, Athanas Peter Kazige na Faustin Peter Bisangwa.

Akizungumza jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wakili Ally Mchungahela alisema mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu umefungwa rasmi na keshokutwa Ijumaa utafanyika mchujo kwa wagombea wote.

Uchaguzi utafanyika Januari 13 2019 kama ulivyopangwa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
6h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’