Mchakato wa kuchukua na kurudisha fomu umefungwa rasmi jana Novemba 19 huku wagombea wengi wakizikwepa fomu za kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa klabu hiyo.
Wakati zoezi hilo likifungwa jana, uongozi wa Yanga umeweka msimamo kuwa utasimamia Katiba ya klabu hiyo na kusisitiza hawatafanya uchaguzi kwa nafasi ya Mwenyekiti.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga Hussein Nyika amesema klabu hiyo inamtambua Manji kuwa Mwenyekiti halali kulingana na Katiba ya klabu hiyo
Amesema Yanga itafanya uchaguzi Januari 13 2019 kama ilivyoagizwa na Mamlaka husika lakini sio kwa nafasi ya Mwenyekiti.
Nafasi nyingine zinazowaniwa ni ya Makamu Mwenyekiti na Wajumbe Wanne wa kamati ya Utendaji.
"Tunawataka Wanachama wetu wawe watulivu kipindi hiki. Kila kitu kitafanyika kwa mujibu wa Katiba yetu," amesema
"Uchaguzi tutafanya kwa nafasi nyingine. Nafasi ya Mwenyekiti haitohusika kwa kuwa timu inaye Mwenyekiti"

ADVERTISE HERE