Winga wa klabu ya Difaa Hassan El – Jadida amesema anaiamini timu yake ya zamani, Yanga SC inaweza kuibuka na ushindi dhidi ya Simba Jumatano na anaiombea kwa Mungu ishinde.
Yanga SC itamenyana na Simba SC kesho Jumatano jioni kuanzia Saa 11:00 katika mchezo wa Ngao ya Jamii kuashiria ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Bara msimu wa 2017-2018.
Msuva amekuwa mchezaji wa Yanga SC tangu mwaka 2012 alipotua Jangwani akitokea Moro United kabla ya kuuzwa Difaa Hassan El - Jadida mapema mwezi huu.
“Ninawaamini, na ninawaombea kwa Mungu washinde,†Msuva ameuambia mtandao wa BIN ZUBEIRY
Yanga imerejea Dar es Salaam leo kutoka kisiwani Pemba ilipokuwa imeweka kambi tangu Jumatatu wiki iliyopita ikitokea Zanzibar ilipolala Jumapili baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandege, ikishinda 2-0 Uwanja wa Amaan.

ADVERTISE HERE