Tarimba agoma kuchukua fomu Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Nov 2018
Tarimba agoma kuchukua fomu Yanga
Licha ya mashabiki na Wanachama wa klabu ya Yanga kumtaka achukue fomu awanie Uwenyekiti wa klabu hiyo, Mkurugenzi wa Utawala na Uwekezaji wa kampuni ya SportPesa Abbasi Tarimba amesema hatagombea.

Tarimba amesema kwa sasa anabanwa na majukumu yake ya kazi hivyo kumfanya asiwe na nafasi ya kuweza kuitumikia Yanga.

"Sina mpango wa kugombea nafasi ya Uongozi Yanga ingawa watu wengi wameniomba nichukue fomu ya Uwenyekiti lakini bahati mbaya majukumu mengi yamenikabili sitoweza," amesema

Mchakato wa kuchukua na kurudisha fomu unafika tamati leo Jumatatu, Novemba 19 2018 huku mpaka juzi Ijumaa kukiwa na wagombea wanne pekee waliokuwa wamejitokeza kuwania nafasi ya Mwenyekiti.

Bado uongozi wa Yanga umesisitiza kutokubaliana na uchaguzi huo kwa upande wa nafasi ya Mwenyekiti baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo Yusufu Manji kukubali kurejea kwenye nafasi yake

Yanga imeitisha Mkutano Mkuu Disemba 01, 2018 ambapo inaelezwa Manji atahudhuria Mkutano huo na kuweka wazi mikakati yake

Miongoni mwa wagombea waliojitokeza kuwania nafasi ya Manji hakuna hata mmoja ambaye anaonekana kuwapa imani Wanachama wa klabu hiyo ambao ndio watakaopiga kura Januari 13 2019.

Hadi juzi jioni, wagombea wanne waliokuwa wamejitokeza kuwania nafasi ya Mwenyekiti ni Dr Jonas Tibaroha, Mbaraka Igangula, Yono Kevele na Titus Osoro.

Kevele na Osoro walichukua fomu mbili, ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti kila mmoja ambapo Kamati ya Uchaguzi ya TFF imesema watatambua fomu moja pekee itakayojazwa na wagombea hao mara watakaporudisha.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
5h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’