FT : Lesotho 1-0 Tanzania

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Nov 2018
FT : Lesotho 1-0 Tanzania
Stars imeshindwa kutamba huko Lesotho baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wenyeji, Lesotho.

Ulikuwa ni mchezo ambao Stars ilihitaji kushinda ili kujihakikishia nafasi ya kutinga fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika nchini Cameroon.

Matokeo hayo sasa yanaifanya Stars kulazimika kushinda mchezo wa mwisho dhidi ya Uganda utakaopigwa March 2019 huku ikiomba Lesotho isipate ushindi kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya Cape Verde ambao watakuwa ugenini.

Lesotho ilitawala mchezo huo kwa muda mwingi huku ikikosa nafasi nyingi kabla ya kufunga baada ya mpira wa kona uliopanguliwa na mlinda lango Aishi Manula kutua kichwani kwa mchezaji wa Lesotho.

Tanzania iliyocheza kwa kujihami zaidi ilikosa nafasi kadhaa kupitia mipira miwili ya adhabu iliyopigwa na Aggrey Morris na nafasi nyingine mbili zikikoswa na Shabani Iddi Chilunda.

Lesotho imepanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi L baada ya kufikisha alama tano sawa na Tanzania.

Licha ya Tanzania kuwa na uwiano mzuri wa mabao, Lesotho imenufaika na sheria ya matokeo ya jumla baina ya timu hizo mbili.

Lesotho imevuna alama nne dhidi ya Tanzania iliyopata alama moja kutoka kwao.

Michezo ya raundi ya sita ndio itaamua ni timu ipi inaungana na Uganda kwenda Cameroon huku Lesotho ikiwa mbele ya Tanzania na Cape Verde yenye alama nne
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’