Nafasi ya Mwenyekiti Yanga bado ni 'kaa la moto' kwa TFF

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
18 Nov 2018
Nafasi ya Mwenyekiti Yanga bado ni 'kaa la moto' kwa TFF
Licha ya Shirikisho la soka nchini (TFF) kusisitiza uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi (ikiwemo ya Mwenyekiti) katika klabu ya Yanga lazima uendelee bado viongozi wa Yanga wameshikilia msimamo wa kupinga uchaguzi huo kwa nafasi ya Mwenyekiti.

Ukitathmini kwa umakini utabaini viongozi hao wana hoja ya msingi kwani TFF walishamtambua Manji kuwa amerejea Yanga kupitia barua yao ya Julai 11 walipomtimua Clement Sanga aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi kwa kuwa alikosa sifa baada ya Manji kurudi

Inashangaza leo TFF kutumia barua ya Manji kujiuzulu kuwa kigezo cha kutomtambua wakati walitumia barua ya Yanga iliyomtambulisha kuwa amerudi kumuondoa Sanga

TFF haipaswi kuwa na maamuzi ya aina mbili katika jambo moja. Kwamba kumuondoa Sanga kwa kuwa Manji amerudi Yanga ni sawa lakini sio sawa Manji kuiongoza Yanga!

Kwamba TFF wametumia maamuzi ya Yanga kwa upande ambao ulikuwa na faida kwao lakini wanayapinga maamuzi hayohayo kwa upande ambao una faida kwa Yanga!

Yanga sio kwamba haiwezi kumshawishi Manji achukue fomu, bali inataka maamuzi yake inayofanya kupitia vikao vyake halali yaheshimiwe

Ni wazi kama Manji akichukua fomu hakuna mgombea mwenye ubavu wa kushindana nae. Atashinda kwa kishindo.

Na TFF hawana uwezo wa kuwapangia Yanga kiongozi kwani watakaopiga kura sio wao, ni wanachama wa Yanga

Mchakato wa kuchukua na kurudisha fomu unaosimamiwa na TFF unafungwa kesho na Manji sio miongoni mwa wagombea waliojitokeza kuchukua fomu kama ilivyopendekeza na TFF.

Jambo hili linahitaji busara ya hali ya juu kulipatia muafaka, ubabe hautasaidia.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
6h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’