Kikosi cha mabingwa kihistoria wa Tanzania Yanga leo Jumapili saa kumi jioni kinashuka kwenye uwanja wa Majaliwa wilayani Ruangwa kuikabili timu ya daraja la kwanza, Namungo Fc.
Yanga iliwasili mkoani Lindi jana jioni na leo asubuhi itajifua kwenye uwanja wa Majaliwa kabla ya mchezo hapo jioni.
Yanga ilisafiri na kikosi chake kamili na kama ilivyokawaida yake kwenye michezo ya kirafiki, kocha msaidizi Noel Mwandila ataendelea na utaratibu wa kuwapa nafasi wachezaji wote.
Mji wa Ruangwa 'ulizizima' jana baada ya Yanga kuwasili na hakuna shaka mashabiki wengi watajitokeza kuwashuhudia mabingwa hao wa kihistoria

ADVERTISE HERE