Wanne wajitokeza kuwania nafasi ya Manji Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Nov 2018
Wanne wajitokeza kuwania nafasi ya Manji Yanga
Hadi jana jioni wagombea 22 walijitokeza kuchukuwa fomu kuwania nafasi mbalimbali za uchaguzi wa klabu ya Yanga huku wanne wajichukua fomu za kugombea nafasi ya Mwenyekiti iliyokuwa inashikilwa na Yusuf Manji.

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) lilisogeza mbele siku za kuchukuwa fomu ambapo sasa zoezi hilo litafungwa Novemba 19 wakati uchaguzi huo utafanyika Januari 13, 2018.

Nafasi ya Mwenyekiti waliojitokeza kuchukuwa fomu hizo wapo wanne hadi jana Ijumaa ambao ni Dr Jonas Tibaroha, Mbaraka Igangula, Yono Kevele na Titus Osoro.

Kevele na Osoro wao wamechukuwa fomu mbili, ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti kila mmoja ambapo Kamati hiyo imesema watatambua fomu moja pekee itakayojazwa na wagombea hao mara watakaporudisha.

Wajumbe waliojitokeza hadi hiyo jana ni Mussa Katabalo, Salim Seif, Benjamini Jackson, Pindu Luloya, Silvester Haule, Hamad Islam, Shaffii Amri, Said Baraka, Dominic Francis, Ally Msigwa, Leonard Malongo, Salum Chota, Ramadhan Said, Geofrey Mwita, Faustine Mabula, Frank Kalokola na Arafati Haji

Kamati hiyo pia itafanya marekebisho ya ratiba ya mchakato mzima wa uchaguzi huo baada ya kuwepo mabadiliko ya kuongeza siku ya kuchukuwa fomu.

"Ratiba nayo itabadilika na tunaifanyia kazi, hivyo lini usaili utafanyika na mambo mengine itajulikana baada ya kamati kupanga, hao waliochukuwa fomu mbili nafasi tofauti wakirudisha itabidi wachague nafasi moja tu, kwani hiyo ndiyo inayokubalika kwani haiwezekani kugombea nafasi mbili mtu mmoja na kwa wakati mmoja," alisema Herman Kidifu ambaye ni mwanasheria na mwanachama wa TFF.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12m ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
3h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
8h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’