Usipate hofu hawa wakianzia benchi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Aug 2017
Usipate hofu hawa wakianzia benchi
Soka mbinu, hicho ndicho kinachosubiliwa kesho wakati makocha wa Yanga, George Lwandamina na mwenzake wa Simba, Joseph Omog jinsi watakavyowatumia wachezaji wao kwa makini katika kuhakikisha wanaondoka na ushindi katika mchezo huo wa Ngao ya Jamii utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Moja ya sifa ya kocha ni jinsi anavyoweza kuwatumia wachezaji wake wa akiba kuingia kubadilisha mchezo na kuisaidia timu kupata ushindi.

Kama wewe ni shabiki basi ondoa shaka unapowaona wachezaji hawa hawamo kwenye kikosi kitakachoanza Yanga kwani wanapoingia huenda wakabadilisha taswira ya mchezo pindi wakitokea benchi.

Donald Ngoma

Anapewa nafasi kubwa ya kuanza katika mchezo wa kesho Jumatano dhidi ya Simba, lakini kutokana na hazina ya washambuliaji ambayo Yanga inayo, Ngoma anaweza kuanza kama mchezaji wa akiba.

Kutokana na uwezo wake mkubwa wa kusoma mabeki wa timu pinzani na kazi aliyonayo, ni wazi kuwa kama ataanzia benchi mechi ya Jumatano, anaweza kuwa tatizo kwa Simba.

Amissi Tambwe

Uwezo wake wa kuamua mechi akiingia kutokea benchi ulijidhihirisha msimu uliopita katika mechi ambayo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya JKT Ruvu.

Katika mchezo huo, Tambwe aliingia na kuifungia Yanga mabao mawili huku mengine yakifungwa na Saimon Msuva na Obrey Chirwa.

Juma Abdul

Abdul ni mmoja wa wachezaji wanaoweza vyema kubadilisha mechi pindi wanapoingia kutokea benchi hasa pale timu inaposaka matokeo.

Msimu uliopita, beki huyo aliingia akitokea benchi kwenye mechi dhidi ya Toto Africans ambayo Yanga walikuwa wanahitaji ushindi ili wajiweke kwenye mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa.

Beki huyo sio tu aliiamsha Yanga bali ndiye aliyepiga krosi iliyozaa bao la ushindi kupitia kwa Amiss Tambwe.

Ibrahim Ajib

Uwezekano mkubwa uliopo ni Ajib kuanzishwa kwenye mechi hiyo lakini hata akiwekwa benchi, bado Simba hawatokuwa salama pindi akiingia.

Uwezo wake wa kupiga faulo, chenga na kumiliki mpira, inaweza kuwa chanzo kwa yeye kubadilisha mchezo iwapo atatokea benchi.

Msimu uliopita, Ajib alitokea benchi kwenye fainali ya Kombe la FA dhidi ya Mbao FC na akawa chanzo kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Kwa hisani ya Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’