Manji 'apigwa stop' kurejea Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Nov 2018
Manji 'apigwa stop' kurejea Yanga
Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Yanga na Kamati ya uchaguzi ya TFF kimefikia makubaliano ya kuendelea na mchakato wa uchaguzi wa kujaza nafasi zote zilizowazi ikiwemo ya Mwenyekiti

Viongozi wa Kamati hizo walikutana leo katika kikao kilichosaka mwafaka wa hatma ya nafasi ya Mwenyekiti baada ya Manji kuandika barua ya kuridhia kurejea kwenye nafasi yake wakati nafasi hiyo ikiwa imetangazwa kuwa wazi.

Akizungumzia maamuzi ya kikao hicho, Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi TFF Malangwe Ally Mchungahela amesema imebainika Mkutano Mkuu wa Yanga hauna uwezo wa kumrejesha Manji katika nafasi yake.

Kufanya hivyo ni kuvunja Katiba ya Yanga.

Amesema kwa mujibu wa katiba ya Yanga, Manji alipoteza nafasi yake baada ya kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu

Amesema Katiba ya Yanga inabainisha kuwa Mkutano Mkuu unaweza kubadili kanuni na kurekebisha katiba yenyewe lakini si kumrudisha kiongozi aliyejiuzulu

Kwa maana hiyo njia pekee kwa Manji kurejea katika nafasi hiyo ni kugombea katika uchaguzi wa Januri 13 2019.

Bado kuna siku tatu kabla zoezi la kuchukua na kurudisha fomu kufungwa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’