Uongozi wa klabu ya Azam FC umerejesha mechi zake ambazo watacheza dhidi ya Simba na Yanga kwenye ligi Kuu Bara msimu huu katika Uwanja wa Taifa, kwa madai ya kushindwa kuhimili Changamoto ya mashabiki katika uwanja wao wa Azam Complex uliopo Chamazi.
Msimu uliopita Azam Fc ilitumia uwanja wake wa Azam Complex katika michezo yote ya nyumbani lakini uongozi wa timu hiyo umedai changamoto ya udogo wa uwanja hasa kwa michezo dhidi ya miamba hiyo ya soka nchini imewalazimu kuhamishia michezo hiyo uwanja wa Taifa.
Hata hivyo wadau wa soka wanaamini suala la mapato linaweza kuwa sababu kuu ya kuhamishia michezo hiyo uwanja wa Taifa
Michezo dhidi ya Simba na Yanga ndio inayoziingizia timu mapato mengi hivyo haitashangaza kuona timu zaidi zikaomba kutumia uwanja huo dhidi ya miamba hiyo ya soka nchini wakati huu ambao timu mwenyeji inachukua mapato yote ya mchezo husika.

ADVERTISE HERE