Yanga, TFF kujadili Uchaguzi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Nov 2018
Yanga, TFF kujadili Uchaguzi
Kamati ya utendaji ya klabu ya Yanga hapo kesho Ijumaa inatarajiwa kuwa na kikao na Kamati ya uchaguzi ya TFF ili kujadili mustakabali wa Uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi.

Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amethibitisha kuwepo kwa kikao hicho ambacho kina lengo la kupata suluhisho juu ya kile kinachoendelea katika klabu ya Yanga hivi sasa.

Jana TFF iliongeza muda wa kuchukua na kurudisha fomu kwa siku tano zaidi ili kuwapa nafasi wagombea wengi waweze kujitokeza.

Mpaka sasa wagombea 21 wamejitokeza kuwania nafasi hizo zinazojumuisha Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji.

Licha ya mchakato huo, uongozi wa Yanga umeendelea kumtambua Mwenyekiti wake Yusufu Manji ambaye alimuandikia barua Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini Kapteni George Mkuchika kumtaarifu kuwa amekubali kurejea klabuni hapo na ataanza kazi rasmi ifikapo January 15, 2019.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
45m ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
4h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
9h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’