Kwa mara ya tatu Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) limeongeza muda wa kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi za uongozi wa klabu ya Yanga sasa zoezi hilo likitarajiwa kufungwa Novemba 19, 2018.
Awali zoezi hilo lilikuwa lifungwe leo Jumatano, Novemba 14, 2018.
Katika hatua nyingine, Kamati ya Utendaji ya Yanga na ile ya uchaguzi ya TFF zinatarajiwa kukutana keshokutwa Ijumaa.
Wakati mchakato huo ukiendelea, Yanga imeitisha Mkutano Mkuu wa dharura Novemba 24 2018 ambapo suala la Uchaguzi huo na hatma ya Mwenyekiti Yusufu Manji zikitarajiwa kuwa miongoni mwa ajenda za Mkutano huo.
Uchaguzi umepangwa kufanyika Januari 13,2019 nafasi zinazowaniwa zikiwa ni Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji.

ADVERTISE HERE