Bossue ameomba kurudi 'kundini'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Nov 2018
Bossue ameomba kurudi 'kundini'
Aliyewahi kuwa beki wa kati wa Yanga, raia wa Togo Vincent Bossou ameomba kurejea ndani ya klabu hiyo kwenye dirisha dogo la usajili, linalotarajiwa kufunguliwa Novemba 15.

Bossou aliichezea Yanga kwa mafanikio ndani ya misimu miwili mfululizo akijiunga na klabu hiyo Agosti 2015 na mara baada ya kumaliza mkataba wake alitimka nchini kutokana na Yanga kushindwa kufikia makubaliano na beki huyo.

Mratibu wa Yanga, Saleh Hafidh amesema amekuwa akiwasiliana mara kwa mara na nyota huyo akiomba kurejeshwa katika kikosini dirisha dogo la usajili ili aendelee kuisaidia timu hiyo ambayo haina msaidizi wa Yondani.

β€œBossou amekuwa akiniomba sana arudi, sasa kwa kuwa kocha hayupo namsubiri arudi ili nimweleze kama atakubali kwa kuwa hata yeye alisema anahitaji kuongeza mchezaji katika nafasi hiyo,” Hafidh amenukuliwa na Mwanaspoti.

Kwa mujibu wa kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mwingi Zahera alikiri kutafuta beki wa kati ambaye ataongeza nguvu kikosini kwake dirisha dogo la usajili linalotarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.

Zahera, ambaye ni kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Congo, yupo nchini Congo wakijiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika mwakani (AFCON 2019) dhidi ya Congo Brazaville, mchezo utakaochezwa Novemba 18 alipotafutwa kwa ajili ya kuzungumzia hilo alisema kwa sasa yupo na majukumu ya timu yake ya taifa na kuombwa kutafuta baada ya kurejea nchini.

β€œHuku pia nipo kazini na nimeomba ruhusa kwa uongozi umenipa nafasi ya kuja kulitumikia taifa langu, ishu za Yanga kwa sasa siwezi kuzipa kipaumbele kwa sababu nipo nje ya majukumu naomba unitafute nikirejea nchini ili niweze kulizungumzia zaidi,” alisema.

Bossou aliyezaliwa Februari 7, mwaka 1986 mjini Kara, Togo, aliibukia klabu ya Maranatha FC ya kwao, kabla ya kusaini Etoile du Sahel ya Tunisia Januari 15, mwaka 2010 mkataba wa miaka miwili.

Nyota huyo alikuwepo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Togo kilichojitoa AFCON ya mwaka 2010 Angola, baada ya basi la wachezaji kushambuliwa na majeshi ya waasi likiwa njiani kwenda kwenye fainali hizo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’