Mawazo huru : Hatma ya Yanga iko mikononi mwa WanaYanga wenyewe

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
13 Nov 2018
Mawazo huru : Hatma ya Yanga iko mikononi mwa WanaYanga wenyewe
Katika pitapita zangu huko mitaani nilikutana na mdau mmoja ambaye alikuwa na maoni tofauti nami kuhusu sakata la uchaguzi wa Yanga na hatma ya Mwenyekiti wa klabu hiyo Yusufu Manji aliyeandika barua ya kukubali ombi la Wanachama waliomtaka arudi kwenye nafasi yake.

Baada ya TFF kutangaza kuanza kwa mchakato wa uchaguzi wa Yanga, licha ya Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini Kapteni George Mkuchika 'kuifichua' barua aliyoandika Manji akiomba arejee uongozini kuanzia Januri 15 2019, kwa kuwa mchakato tayari umeanza, wengi tunaamini ni vyema uchaguzi huo ukaendelea na Manji anaweza kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo.

Lakini mdau huyu yeye ana mtizamo tofauti;

Kwanza anaunga mkono kwa asilimia 100 hatua ya uongozi wa Yanga kuendelea kumtambua Manji baada ya yeye mwenyewe kuandika barua ya kukubali kurudi katika nafasi yake.

Manji alichaguliwa na Wanachama wa Yanga kupitia Mkutano Mkuu. Kwa sasa muda wake bado haujamalizika na licha ya kuomba kujiuzulu (kutokana na changamoto zilizomkumba), bado wanachama walimuomba asiachie nafasi yake kwa kuwa wanamuamini.

Na kwa kuwa mwenyewe sasa amekubali ombi hilo la Wanachama, kwa mujibu wa Katiba ya Yanga yeye ni Mwenyekiti halali na itakuwa kituko kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi ya Mwenyekiti ambaye yupo!

Kwa mujibu wa Katiba ya Yanga, nafasi ya Mwenyekiti itakoma kama; a) muda wa uongozi umekwisha, b)Kifo, c)kujiuzulu, d)kuondolewa na Wanachama

Aidha, ombi la kujiuzulu ni lazima lipitishwe na Wanachama. Wanachama wasiporidhia, utaendelea kutambuliwa hata kama umejiuzulu mpaka pale muda wako utakapokwisha

Pili mdau huyu anasema Yanga inamuhitaji sana Manji wakati huu ambao inaelekea kwenye mchakato wa kufanya mabadiliko.

Alitolea mfano klabu ya Simba kuwa imefanikiwa kufanya mabadiliko kwa urahisi kwa kuwa tayari ilikuwa na Bilionea Mohammed Dewji 'MO'.

Mdau huyu anasema ukifuatilia mchakato wa mabadiliko wa Simba kilichobadilika kwenye makaratasi ni mfumo wa uendeshaji tu lakini kiuhalisia timu hiyo bado inamtegemea MO kwa kila kitu kama ilivyokuwa awali kabla hawajabadili mfumo wa uendeshaji.

Anasema Yanga nayo inamuhitaji Manji kwa kuwa ndiye mpaka sasa aliyeonyesha kuwa na mapenzi ya kweli kwa klabu hiyo.

Manji amekuwa sehemu ya familia ya Yanga kwa zaidi ya miaka 10 na amekuwa akitumia mabilioni yake kuipa mafanikio timu hiyo.

Mdau huyu akaniuliza swali : Ni nani aliyejitokeza kuisaidia Yanga wakati Manji alipokumbwa na matatizo?

Mimi nikamjibu : HAKUNA

Mdau akaongeza : Umeona madhara yaliyotokea baada ya Manji kukaa pembeni? Timu imepoteza ubingwa, usajili umekuwa wa tabu, wachezaji hawalipwi mishahara kwa wakati, viongozi wanajiuzulu kila kukicha.

Mdau anasema Wanachama wa Yanga wanafahamu changamoto hizi kwani ziko dhahiri. Leo hii akina Mzee Akilimali na wengineo ambao wanapaza sauti zao kumkataa Manji wakati timu ikiwa kwenye hali ngumu huwaoni.

Hawako tayari kutoa hata senti tano kuisaidia timu. Timu imekumbwa na hali ngumu ya kiuchumi mpaka kufikia hatua ya kuomba kuchangiwa na wanachama na mashabiki wake. Hukuona bilionea yeyote aliyejitokea kuisaidia timu zaidi ya Manji.

Kwani licha ya kuwa nje, Manji ameendelea kutoka msaada wa hali na mali.

Mdau huyo amewaasa WanaYanga wawe makini sana kwani mgogoro unao-onekana kuikumba timu hiyo ni wa kutengenezwa na utawanufaisha zaidi wapinzani wao na wale wasiopenda Yanga ifanikiwe.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’