Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kinaendelea kujifua nchini Afrika Kusini kujiandaa na mchezo kusaka tiketi ya kufuzu kwa fainali za michuano ya AFCON 2019 dhidi ya Lesotho.
Mchezo huo utapigwa Jumapili ijayo, Novemba 18 huko Masseru, Lesotho.
Afisa Habari wa TFF Clifford Ndimbo amesema wachezaji wa Kimataifa wanaocheza nje ya Tanzania wameanza kuwasili nchini Afrika Kusini kujiunga na wenzao tangu jana.
Hassani Kessy, Abdi Banda na Rashidi Mandawa wamejiunga na kambini jana wakati kiungo Himid Mao na wachezaji wengine wanatarajiwa kuwasili leo
Ndimbo amesema wachezaji Beno Kakolanya na Yahya Zayd waliokuwa majeruhi wamepona na tayari wamerejea mazoezini.
Stars inajifua kwenye uwanja wa Bloemfontein Celtic kujiandaa kabla ya kuikabili Lesotho katika mchezo ambao matokeo ya ushindi kwa Stars huenda yakaipeleka timu hiyo fainali za AFCON kwa mara ya kwanza baada ya kusubiri kwa zaidi ya miaka 35

ADVERTISE HERE