Aliyepitishwa kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Thobias Lingalangala, amekubali kuachia nafasi hiyo baada ya Yusuf Manji kuandika barua ya kurudi.
Akizungumza jana baada ya mkutano wa baraza la wadhamini kumalizika, Lingalangala alisema hana sababu ya kuendelea kukaimu nafasi hiyo kwani katiba haimruhusu.
"Barua tayari imeshaandikwa na Mwenyekiti kwamba anarejea kwa hiyo mimi nawezaje kukaimu nafasi hii, nilikaimu kwa sababu mwenyekiti hakuwepo na si vinginevyo," Lingalangala aliuambia mtandao wa Mwanaspoti
Mapema Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini, George Mkuchika, alisema nafasi ya Lingalangala ilikoma baada ya Manji kuandika barua ya kurejea.
Mkuchika alisema Lingalangala ameiridhia barua ya kurejea kwa Manji na hakuna tofauti yoyote baina yake na viongozi wengine wa Yanga
"Lingalangala hana tofauti yoyote hata na Lukumay wala sisi, tayari wameshashikana mikono na tupo nae pamoja sisi Yanga ni watu wa moja," alisema.

ADVERTISE HERE