Mkuchika athibitisha Manji amerejea Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Nov 2018
Mkuchika athibitisha Manji amerejea Yanga
Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la klabu Yanga Kapteni George Mkuchika amesema Yussuf Manji amerejea katika nafasi yake baada ya kumuandikia barua ya kukubali ombi la Wanachama wa klabu hiyo kumtaka atengue uamuzi wake wa kujiuzulu

Akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kikao kilichoitishwa na Baraza hilo, Kapteni Mkuchika ameonyesha barua iliyoandikwa na Manji kuridhia kurejea katika nafasi ya Uwenyekiti wa Yanga huku akiomba kuanza kazi rasmi ifikapo Januari 15, 2019.

Kapteni Mkuchika amesema Manji aliandika barua ya kujiuzulu lakini wanachama walilikataa ombi lake kupitia Mkutano halali wa klabu hiyo na kumuomba arejee katika nafasi yake.

Barua hiyo aliyoandika ni uthibitisho kuwa ameridhia maombi ya wanachama wa Yanga na sasa ni rasmi amerejea katika nafasi yake.

Kapteni Mkuchika amesema Manji ndio Mwenyekiti wa Yanga huku Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Thobas Langalanga aliyekuwa ameteuliwa kukaimu wadhifa huo hatambuliki
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’