Klabu ya Singida United iliyopanda daraja misimu miwili iliyopita na kuleta ushindani mkali katika msimu wake wa kwanza, imekumbwa na ukata unaohatarisha mustakabali wa timu hiyo.
Mfadhili na Mlezi Mkuu wa timu hiyo, Dk Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mdau mkubwa wa Yanga, amekiri kuwa Singida United inakabiliwa na changamoto za kiuchumi.
Mpaka sasa wachezaji watatu wamevunja mikataba yao huku wengine zaidi ya sita wakiwa mbioni kufanya hivyo ili waweze kusajiliwa na timu nyingine wiki ijayo dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa.
Miongoni mwa wachezaji walioomba kuvunja mkataba ni Tiber John winga aliyesajiliwa na timu hiyo kutoka Ndanda Fc.
Yanga ilijaribu kumsajili winga huyo mwezi Julai hata hivyo aliikataa ofa ya Yanga na kuamua kujiunga na Singida United
Timu hiyo imekumbwa na ukata baada ya wadhamini waliokuwa wanaiunga mkono 'kuingia mitini'.
Baadhi ya wachezaji wanadai hawajalipwa mshahara kwa zaidi ya miezi mitatu

ADVERTISE HERE