Huyu Tarimba tumshawishi achukue fomu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Nov 2018
Huyu Tarimba tumshawishi achukue fomu
Mchakato wa uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi katika klabu ya Yanga umeanza rasmi jana ambapo fomu zilianza kutolewa Ofisi za TFF Ilala jijini Dar es salaam na Makao Makuu ya klabu ya Yanga.

Nafasi zilizotangazwa kuwaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na nafasi nne za wajumbe wa Kamati ya utendaji.

Mwisho wa zoezi la kuchukua na kurudisha fomu ni Novemba 13, 2018 hivyo kuna takribani siku nne zimebaki kabla ya zoezi hilo kufungwa Jumanne ijayo.

Wagombea wenye sifa wametakiwa kujitokeza kuchukua fomu lakini pia inaruhusiwa kuwashawishi na hata kuwachukulia fomu wagombea ambao tunadhani wanaweza kuiongoza kwa mafanikio klabu ya Yanga.

Mimi binafsi ninamshawishi Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya SportPesa Bw. Abbas Tarimba achukue fomu na nitawashawishi Wana Jangwani wenzangu wampigie kura aweze kuiongoza Yanga

Tarimba anao uzoefu wa kutosha kuiongoza Yanga. Amewahi kuwa Mwenyekiti wa Yanga miaka ya nyuma na mmoja wa viongozi walioanzisha vuguvugu la mabadiliko katika klabu ya Yanga.

Haikutokea kama bahati mbaya kwa Baraza la Wadhamini kumpendekeza kuongoza Kamati Maalum iliyoundwa mapema mwaka huu kuinusuru Yanga

Kwa kiasi kikubwa Tarimba aliwezesha kufanikisha usajili wa baadhi ya wachezaji waliokuwa wanaondoka wakati wa dirisha kubwa la usajili ingawa Kamati yake ilishindwa kufanya kazi baada ya kupingwa na baadhi ya viongozi wa Yanga

Wakati wa uongozi wake akishirikiana na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga, marehemu George Johnson Mpondela β€˜Castro’, walianzisha vuguvugu la kutaka kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu ya Yanga na kuwa Kampuni.

Jitihada zao hizo zilisababisha kuibuka kwa mgogoro mkubwa uliopelekea kuigawa Yanga katika makundi mawili; Yanga Asili waliokuwa wakipinga mabadiliko na Yanga Kampuni waliokuwa wakiwaunga mkono Tarimba na Castro.

Ni zaidi ya miaka 20 sasa imepita na bado Yanga imeshindwa kufikia maono yake lakini tayari timu kama Simba imetekeleza kile alichokuwa akikiona siku hizo.

Naamini WanaYanga wote wako tayari kwa mabadiliko, ni wachache sana ambao wataendelea kupinga kutokana na uhalisia wa nyakati tulizonazo.

Yanga inahitaji kiongozi ambaye ajenda yake ya kwanza iwe ni mabadiliko ili kuiondoa Yanga hapa ilipo.

Miongoni mwa watu wanaoweza kuifanya kazi hiyo kwa ufasaha, Tarimba ni mmoja wao. Kwani tayari ana uzoefu kupitia jaribio lake lililokwama zaidi ya miaka 20 iliyopita



Pia Yanga inao watu makini kama Ally Mayay, Mh Ridhiwani Kikwete, Auron Nyanda, Bin kreb, Seif magari na wengineo wengi wenye mapenzi mema na uwezo wa kuipeleka Yanga mbele

Hawa wote tuwashawishi wachukue fomu ili tuwape mamlaka ya kututoa hapa tulipo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’