Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika amesema wamejipanga kutimiza maagizo yote ya usajili walioachiwa na kocha Mwinyi Zahera dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa wiki ijayo.
Taharuki iliwakumba mashabiki wa Yanga jana baada ya mmoja wa washambuliaji waliokuwa wanatarajiwa kusajiliwa, Obrey Chirwa kutambulishwa na klabu ya Azam Fc baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja.
Hata hivyo Nyika amesema Chirwa hakusajiliwa Yanga kwa kuwa jina lake sio miongoni mwa majina yaliyopendekezwa na Zahera ili asajiliwe.
Zahera ambaye tayari ametimkia DR Congo kutimiza majukumu ya timu ya Taifa yeye akiwa kocha msaidizi, alipendekeza usajili wa wachezaji wanne wa Kimataifa wakati wa dirisha dogo.
Hata hivyo wengi wamekuwa na wasiwasi kuwa huenda Yanga ikashindwa kufanikisha usajili huo kutokana na hali ya ukata inayoikabili klabu hiyo
Nyika amewahakikishia WanaYanga kuwa dirisha la usajili litakapofunguliwa watafanya kama walivyoagizwa na kocha wao.
"Dirisha la usajili bado halijafunguliwa kwasasa tuko 'bize' kuiandaa timu iweze kupata matokeo mazuri michezo yake yote iliyobaki.
"Muda wa usajili ukifika tutasajili kama maelekezo ya mwalimu yalivyo.
"Kuhusu ukata katika timu hiyo ni ishu nyingine baina ya timu na viongozi hatuwezi tukakwambia sasa tuna pesa au hatuna," alisema Nyika.

ADVERTISE HERE