Sina kinyongo na Zahera - Chirwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Nov 2018
Sina kinyongo na Zahera - Chirwa
Baada ya kutua Azam Fc mshambuliaji wa zamani wa Yanga Obrey Chirwa amesema hana kinyongo na kocha wa timu hiyo Mwinyi Zahera aliyemuwekea ngumu kurejea Jangwani.

"Kocha alisema mimi simtaki Chirwa sababu ana tabia ya kugoma. Ni kweli mimi niko hivyo hivyo na siwezi kubadilika," Chirwa aliwaambia waandishi wa habari jana baada ya kutambulishwa na Azam Fc.

"Mpira ni kazi yangu, kama silipwi stahiki zangu lazima nidai kwa njia yoyote. Na kama nikishindwa nitavunja mkataba"

"Sina tatizo na kocha wala klabu ya Yanga, ninamtakia kila la kheri aweze kuipa mafanikio Young Africans," amesema

Katika hatua nyingine Chirwa ameeleza kushangazwa na wachezaji wengi hapa nchini kutokana na kushindwa kuwa na misimamo jambo ambalo linawafanya waendelee kuzipigania timu zao bila kulipwa chochote.

"Unajua wachezaji wengi hapa nchini wamekosa msimamo wa kulinda mikataba yao, niko tayari kuvunja mkataba wangu na kwenda mahala pengine ninapoona stahiki zangu hazilipwi kwasababu nina familia na inanitegemea" alisema.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’