Ridhiwani awashukia wanaopinga Uchaguzi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Nov 2018
Ridhiwani awashukia wanaopinga Uchaguzi Yanga
Aliyekuwa mmoja wa Wajumbe wa kamati Maalum iliyoundwa kuinusuru Yanga, Mh. Ridhiwani Kikwete (MB) amewashukia wanachama wa klabu hiyo wanaopinga kufanyika kwa uchaguzi ambao mchakato wake tayari umetangazwa na TFF.

Jana baadhi ya Wanachama wa Yanga wakiongozwa na Mwenyekiti wa Matawi Bakili Makele walikutana kwa dharura ambapo walitoa tamko la kupinga uchaguzi wa Yanga kusimamiwa na TFF huku pia wakisisitiza bado wanamtambua Yusufu Manji kama Mwenyekiti wa klabu hiyo.

Miongoni mwa nafasi zilizoagizwa kufanyiwa uchaguzi katika klabu ya Yanga ni nafasi ya Mwenyekiti.

Nafasi nyingine ni ya Makamu Mwenyekiti na Wajumbe Wanne wa Kamati ya Utendaji.

"Mnapofika hatua kama hii ni Dalili kuwa Hamjui Mnachokitaka. Uchaguzi ni Utaratibu wa Kawaida. Mnayemtaka mnaweza kwenda mchukulia fomu," ameandika Mh. Ridhiwani kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram

"Hakuna Busara ya kushindana Ubavu na Wasimamizi wa Mpira TFF. Twendeni tukafanye Uchaguzi. Tunasimamisha Maendeleo ya Timu yetu kwa Ushabiki Usio na Macho ya Kujua Kesho yetu ikoje.

"Mwisho tutakuja tafuta Mchawi,Wakati Wachawi ni Sisi Wenyewe. Tusiwape Kichwa wakatamba," amesema

TFF imetangaza kuanza kutoa fomu kwa wagombea kuanzia kesho Novemba 08 Makao Makuu ya klabu ya Yanga na ofisi za Shirikisho hilo Ilala jijini Dar es salaam.

Mchakato wa uchaguzi utahitimishwa Januari 13, 2019 ambapo uchaguzi huo utafanyika.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’