Chirwa ana kesi ya kumsukuma mwamuzi - TFF

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
21 Aug 2017
Chirwa ana kesi ya kumsukuma mwamuzi - TFF
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemzuia kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mzambia Obrey Chirwa kucheza mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumatano.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema leo katika mkutano na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam kwamba, Chirwa hawezi kucheza kesho kwa sababu katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mbao FC alimsukuma refa mjini Mwanza.

“Chirwa atakukosa mchezo wa Jumatano dhidi ya Simba utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa saa 11:00 mjini Dar es Salaam kutokana na kesi inayomkabili ya kumsukuma mwamuzi aliyechezesha mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu dhidi ya Mbao FC,”alisema.

Lucas amesema mshambuliaji aliyejiunga na Yanga msimu uliopita kutoka PF Platinums ya Zimbabwe amesema atalazimika kuendelea kuwa nje hadi hapo Kamati ya Masaa 72 itakapokutana na kutoa maamuzi dhidi yake.

Pamoja na Chirwa, ambaye hata hivyo ni majeruhi na hayupo kambini kisiwani Pemba, wengine watakoukosa mchezo huo upande wa Yanga ni maheruhi ni kipa Beno Kakolanya na kiungo Goffrey Mwashiuya.

Lucas amewataja marefa watakaochezesha mechi hiyo ni Elly Sasii kutoka Dar es Salaam, atakayesaidiwa na Ferdinand Chacha na Hellen Mduma.

Viingilio katika mchezo huo ni Sh. 7,000 kwa viti vya rangi ya kijani na bluu, 10,000 Viti vya Orange, 20,000 kwa VIP B ba 25 kwa VIP A
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE →
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE →
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE →
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE →
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE →
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →