Mwenyekiti wa Matawi Yanga kuhojiwa na Kamati ya Maadili TFF

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Nov 2018
Mwenyekiti wa Matawi Yanga kuhojiwa na Kamati ya Maadili TFF
Mwenyekiti wa Matawi ya klabu ya Yanga Bakili Makele ameitwa na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la soka la Tanzania (TFF) kuhojiwa kwa nini anapinga agizo lililotolewa na shirikisho hilo kuhusu mchakato wa uchaguzi wa Yanga.

Jana TFF kupitia Kamati yake ya Uchaguzi ilitoa ratiba ya mchakato mzima wa uchaguzi unaotarajiwa kuanza Alhamisi Novemba 08 na kuhitimishwa Januari 13 2019 uchaguzi utakapofanyika.

Viongozi wa matawi ya klabu ya Yanga wakiongozwa na Bakili, wamepinga uchaguzi huo kusimamiwa na TFF wakati timu yao ina Kamati yake ya uchaguzi inayojitosheleza.

Hata hivyo taarifa ya TFF imeeleza kuwa imechukua hatua hiyo kutokana na mapungufu ya kamati ya utendaji na mapungufu ya kamati hiyo ya uchaguzi ya Yanga.

Lakini pia ni kwa kuzingatia maelekezo ya Baraza la Michezo la Taifa ambalo liliagiza uchaguzi huo usimamiwe na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kushirikiana na Uongozi wa Yanga
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’