Matokeo ya sare ya bao 1-1 iliyopata Yanga juzi dhidi ya Ndanda hayawakuwafurahisha mashabiki wa timu hiyo hasa ikizingatiwa mchezo huo ulichezwa dimba la nyumbani, Taifa
Hata kocha mwinyi Zahera hakufurahishwa na matokeo hayo ambapo baada ya mchezo huo aliwashushia lawama washambuliaji wake kwa kushindwa kutumia nafasi nyingi walizopata.
Hata hivyo Yanga bado inaweza kuwa juu ya wapinzani wake Azam Fc na Simba kama itafanikiwa kushinda michezo yake ya viporo.
Yanga kuimarika zaidi baada ya usajili
Baada ya kubaini mapungufu ya kikosi chake, Zahera ana nafasi ya kukiimarisha wakati wa dirisha dogo la usajili linalofunguliwa Novemba 15 2018.
Kwa sasa ligi imesimama kuwapa nafasi wachezaji wa Yanga, Simba na Azam Fc walioitwa Stars kuingia kambini nchini Afrika Kusini.
Mchezo wa Stars dhidi ya Lesotho utapigwa Novemba 18, wakati huo dirisha dogo la usajili tayari litakuwa limefunguliwa.
Kama Yanga itafanikiwa kumalizana kwa wakati na wachezaji itakaowasajili basi wanaweza kuitumikia timu hiyo kwenye mchezo wa kiporo dhidi ya Mwadui Fc utakaopigwa mkoani Shinyanga Novemba 21
Ijumaa iliyopita Zahera aliwaambia waandishi wa habari kuwa Yanga iko mbioni kusajili wachezaji wanne wa kigeni na wengine wazawa kuimarisha kikosi chake.
Alisema uongozi wa timu hiyo ulikuwa katika hatua za mwisho kukamilisha mazungumzo na wachezaji hao ambao alitaja nafasi wanazocheza kuwa na mlinzi wa kati, kiungo, winga na mshambuliaji.
Juzi baada ya mchezo dhidi ya Ndanda Zahera aliweka msisitizo kuwa timu yake ina matatizo ya washambuliaji hasa wa pembeni.
Alisema mawinga wa timu hiyo wote wameshindwa kwendana na falsafa yake ya soka analotaka.
"Hii ndio sababu unaona leo anaweza kucheza Kaseke kwenye nafasi hiyo, mchezo mwingine anacheza Ngasa au Raphael. Kuna sababu ya kutafuta winga ambaye atafiti kwenye falsafa yangu, kwa sasa bado sina mtu sahihi,β alisema Zahera

ADVERTISE HERE