Mabadiliko hayakwepeki Yanga

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
5 Nov 2018
Mabadiliko hayakwepeki Yanga
Watani zetu Simba jana wameanza rasmi kuendesha klabu yao kwa mfumo wa kampuni.

Timu hiyo ilimtangaza Mkurugenzi wa kampuni na ikachagua Mwenyekiti na Wajumbe watano wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo ya Simba Sport Club.

Hii ni hatua kubwa sana iliyopigwa na Simba ambayo hakika kama uongozi wa Yanga utendelea 'kupiga danadana' suala la mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo, hakika tutakuwa tumeridhia kwa hiari yetu kuukabidhi ufalme wetu wa soka la Tanzania kwa miaka mingi.

Tutawezaje kushindana na timu ambayo jana imetangaza kutenga bajeti ya Bil 6.3 kwa msimu huu huku ikipanga kutumia takribani Mil 750 wakati wa usajili wa dirisha dogo unaofunguliwa Novemba 15?

Ni wakati sasa wanachama wa klabu ya Yanga wakaachana na mawazo 'mfu' ya kumtegemea mtu mmoja kuiendesha Yanga.

Najua wengi bado wanapenda kumuona Manji akiendelea kuifadhili Yanga kutokana na mapenzi yake kwa klabu hii.

Lakini nadhani ingependeza zaidi kama Manji atarejea Yanga akiwa Mwekezaji sambamba na Wawekezaji wengine wakiwemo wanachama wa Yanga

Mpira wa sasa unahitaji uwekezaji mkubwa wa kifedha ili kuweza kupata mafanikio endelevu.

Huko tunakoelekea hakuna namna Yanga itaweza kushindana na Simba au hata Azam Fc kama sisi tutaendelea kung'ang'ania mfumo huu wa 'kutembeza bakuli' kwa mashabiki na wanachama.

Ikumbukwe Yanga ndio klabu ya kwanza kupitisha mabadiliko ya mfumo wake wa uendeshaji. Tayari katiba ya klabu ya Yanga inatambua mfumo wa uendeshaji wa kampuni.

Lakini kwa miaka mingi Yanga imeshindwa kutekeleza kwa vitendo mabadiliko hayo kutokana na migogoro ya uongozi inayojitokeza mara kwa mara.

Kwa zama hizi, jambo hilo halihitaji mjadala tena. Tukubali kubadilika tuwe na nguvu za kiuchumi kama wenzetu au tuendelee kubaki na mfumo wetu na kuwa wasindikizaji wa wenzetu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
8m ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’