Zahera anasubiri urejeo wa Banka

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Nov 2018
Zahera anasubiri urejeo wa Banka
Adhabu ya kiungo Mohammed Issa 'Banka' aliyefungiwa miezi 14 na Kamati ya kuzuia na kupambana na dawa zisizo ruhusiwa michezoni ya kanda ya tano Afrika (RADO), inamalizika Februari 08 2019.

Kwa sasa Banka haruhusiwi kujihusisha na maswala yoyote ya soka lakini ataruhusiwa kuanza kujifua na Yanga mwezi wa kwanza, ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya adhabu yake kumalizika.

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amekiri kiungo huyo alimuweka kwenye mipango yake aliposajiliwa hivyo kukosekana kwake kulimvurugia mipango.

Zahera amesema Banka ana uwezo mkubwa na anaamini atakuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Yanga atakaporejea.

"Siwezi kufurahi kumkosa Banka ni mtu niliyekuwa namuhitaji sana hapa Yanga wakati anasajiliwa nilijua kwa aina yake ni wapi nitamtumia," Zahera amenukuliwa na Mwanaspoti

"Unajua Banka anaweza kucheza nafasi nyingi,anacheza kwa juhudi sana pia ana akili sana hayo ni mambo ambayo nayakosa sasa kwa kuendelea kumkosa."
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
20h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’