Chikupe afurahia kurejea kikosini Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Nov 2018
Chikupe afurahia kurejea kikosini Yanga
Beki wa Yanga, Andrew Vincent Chikupe amesema amefurahi kurejea tena uwanjani kuisaidia timu yake kupambana kusaka ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu baada ya kumaliza adhabu na vile vile afya yake kuimarika.

Chikupe kwa sasa yupo fiti baada ya kupona majeraha yake na pia kumaliza adhabu yake aliyokuwa amepewa na kamati ya nidhamu ya TFF.

Amesema alikuwa anaumia kukaa nje akiwaangalia wenzake alivyokuwa akipambana katika mechi za Ligi Kuu.

"Kwa sasa nipo fiti na najipanga kuanza tena kuipigania timu yangu, nashukuru wanayanga wamekuwa pamoja na mimi katika kipindi chote nilichokuwa majeruhi na nikitumikia adhabu yangu," alisema Chikupe.

Beki huyo aliongeza kuwa, kwa sasa akili yake anailekekeza katika michezo ijayo kuanzia wa kesho watakapoikaribisha Ndanda FC kutoka Mtwara.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema Chikupe amefanya mazoezi kwa siku tatu na huenda atamtumia kwenye mchezo wa kesho hasa ikizingatiwa nahodha Kelvin Yondani atakosekana kwa kuwa ni majeruhi.

Katika msimamo wa ligi, Yanga inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 25 ikiiacha Simba kwa pointi mbili inayoshika nafasi ya tatu, Azam FC wanaongoza baada ya kujikusanya pointi 27.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
47m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’